MISINGI YA KUFIKIA MAFANIKIO YA KIUCHUMI
Ninakusalimu tena kwa jina la Yesu !
Katika maisha ya mwilini wakristo tunatakiwa kuwa namafanikio
mazuri ili tuweze kutimiza kusudi la Mungu. Mfano
Isaya 58:7-12, Mathayo 25:35-36 . Huu ndio msingi wa mafanikio haya:
a. Akili/fikra
Fikra
ni mkusanyiko na mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo wa kiutekelezaji
ndani ya mtu. Fikra inaonyesha ulivyo kimaisha. Inaonyesha kiwango chako cha kufikiri
kilipo au kilipofika.
Ni
ukweli kwamba kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote
wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanaozitumia kwa faida na malengo na
kupata mafanikio pia wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha ya shida
hadi wanakufa kwa umaskini. Tuzitumie akili zetu katika kujituma
na kufikiri kwa utofauti na wanavyofiki wengine. Tuwe tayari kujifunza kwa
wenye elimu juu ya kile tunataka kufanya na sio kuiga wanavyofanya watu
wengine.
1Wakorintho 15:34
Katika
kuitumia akili ndipo huonekana tofauti ya wanaojua na wasiojua kitu. Ili
ufanikiwe lazima akili zako utumie kufikiri na kuamua ni nini ufanye, namna
gani na wakati gani. Ili kuonyesha matumizi sahihi ya akili kila binadamu
anatakiwa kufikiri na kuwaza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote katika maisha
yake.
b. Muda.
Kila
binadamu ana muda na amepewa muda wa kuishi na kufanya mambo yake kwa uhuru na
amani. Lakini si watu wote wanaoutumia muda wao vizuri katika kujipatia
mafanikio.
Muda
ndio rasilimali muhimu kuliko zote ukiutumia vizuri hakika utafanikiwa. Jiulize
kuna tofauti gani kati ya tajiri na masikini katika muda? Kila mtu ana masaa 24
tofauti ni matumizi tu
Ukafatilia
utagundua, tajiri ana panga malengo na mipangilio yake katika siku wakati
maskini hana mipangilio. Jiangalie vizuri unatumiaje muda wako ili kuyafikia
mafanikio yako unayotamani uwe nayo. Kuna uhusiano mkubwa kati ya muda na
uthamani katika kufikia malengo yako na usipoangalia utajikuta mafanikio yako
hayaji kwa wakati.
c. Kipawa / kipaji.
Huu
ni uwezo wa ndani alionao kila binadamu bila kujali kabila lake au rangi yake
ana kile anachoweza kukifanya tofauti na wenzake. Hicho ndicho kipaji na mtu
akikigundua na kukitumia vizuri hupata mafanikio.
Kipawa ni kama
kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa. Mithali
17:8
Siku
zote tafuta kujua kipaji chako na kitumie upate utajiri na mafanikio katika
maisha yako. Unapokuwa na kipaji na ukikitumia ipasavyo mafanikio makubwa
yanakuwa upande wako.
d. Nguvu.
Kila
mtu amepewa nguvu na uwezo wa kufanya jambo fulani. Tunaweza kuzitumia nguvu
zetu katika kilimo, biashara na hata kazi yeyote halali na kujipatie kitu tunachataka
katika maisha. Si rahisi tulale tuamke kesho matajiri bila kufanya kazi.
Vijana
wengi utakuta wanataka kufanya kazi rahisi na kupata faida kubwa. Mafanikio ni
mchakato, ni safari. Hivyo ili upate utajiri kubali kutumia nguvu zako.
e. Watu.
Kila
mtu iwe kwa kutaka au kutotaka amezungukwa na jamii ya watu. Na kimsingi
umepewa watu hao na Mungu ili uweze kuwatumia na kupata kile unachotaka/kuhitaji
katika maisha yako.
Lakini
kutokana na watu hawa unaweza na unapaswa uwatumie katika ushauri na maarifa
waliyonayo ili kupata kile unachotaka ambacho si kingine ni mafanikio.
Kushindwa kwako kuwatumia watu hawa hili litakuwa ni tatizo lingine ambapo
ukishindwa kufanikiwa usimlaumu mtu.
Kwa
kuwa na vitu hivyo unakuwa na msingi mkubwa wa kufanikiwa, na hivyo katika
kufanikiwa uvumilivu ni sifa moja wapo ya mtu anayetaka kufanikiwa. Aliye mwaminifu
katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye
dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali
ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? (Luka 16:10-11)
Pamoja na kuwa na vitu hivi vya msingi bila mambo haya bado utabaki kama ulivyo.
1.Kuwa na maono.
Maono ni picha ya maisha yako ya baadaye au
Ni picha kubwa ya namna unavyoona baadaye yako.
The big picture of the preferable future.
Mwanzo 29:15-20,
Mwanzo 21:14-19, Waefeso 1:15-19
Usipoona picha ya baadaye au usipopanga namna
uunavyotaka baadaye yako iwe unachokifanya ndicho
kitakachoamua baadaye yako. Mungu hakupi kitu
usichokiona. AngaliaMwanzo 13:14
2. Kuwa na malengo
- Malengo, Husababisha msaada wa Mungu kutokea Ayubu 22:28
- Malengo hukupa nidhamu ya kimaisha Mwanzo 29:16-18, Mithali 29:18
Mipango na Bajeti
Upangaji mipango ni mchakato unaoweka malengo, kubainisha rasilimali
zilizopo/uwezo na mikakati itakayotumika kufikia malengo katika kipindi
maalumu. Mara uandaaji wa mpango unapokamilika kinachofuata ni utekelezaji. Katika utekelezaji baadhi ya malengo
yaliyowekwa katika mpango yanafikiwa na mengine hayafikiwi katika muda
uliokusudiwa. Pia kadiri wakati unavyoenda ndiyo vipaumbele vipya vinavyoibuka
kutokana na mabadiliko katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi. Hivyo basi, ipo haja ya kufanya mapitio mara
kwa mara ili kuihuisha mipango, kwa kubaini utekelezaji ulipofikia na kuingiza
vipaumbele vipya. Kwa msingi huu,
mapitio ni sehemu muhimu katika mchakato wa upangaji mipango.
Madhumuni ya kupanga
• Kuwezesha utekelezaji wa shughuli katika
utaratibu unaokubalika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
• Kuweza kufahamu
rasilimali zilizopo ili kukabiliana na Vikwazo.
• Kuweza kubinisha mahitaji ya Jamii.
Faida za kupanga
• Kupanga kunawezesha
mgawanyo muafaka wa rasilimali chache zilizopo
• Kupanga kunawezesha utekelezaji wa shughuli
kwa wakati.
• Mpango ni zana inayoongoza katika
usimamizi wa shughuli za maendeleo.
Umebarikiwa kwa kuwa una maono.Tembea katika hayo ufanikiwe.